NYUMBA NANE ZINAZOELEA KWENYE MAJI ULIMWENGUNI



Kuna kitu cha uasi na cha kibinafsi kuhusu kubadilisha maisha ya kuishi kwenye jengo la matofali lilinakshiwa kwa chokaa na kwenda kuishi maisha rahisi, yasiyo ya kawaida kwenye boti. Wakazi wengi wanaoishi kwenye mashua wanafurahia na kuishi maisha yenye msisimko na, kwa kuishi kwao mbali na miji ama vijijini, wanajina kihisia wako katika hali moja na asili.

Kutoka Nchi za Scandinavia hadi Marekani, watu wanatafuta uhuru na jamii wanaoishi kwenye maji. Hapa Dominic Lutyens kupitia kitabu cha Making Waves: Floating Homes and Life on the Water kilichoandikwa na Portland Mitchell, anaangalia mifano ya minane ya boti zilizogeuzwa nyumba za ajabu kote ulimwenguni.


Nyumba ya Max McMurdo ni ushahidi tosha wa aina mbalimbali za boti zilizogeuzwa nyumba ambazo zimeibuka katika muongo mmoja uliopita. Takriban miaka saba iliyopita alibadilisha kontena la ukubwa wa mita 12 kwa 2m ambalo alinunua kwa £2,000 ($2,500) katika eneo la viwanda la London, na kutengeneza nyumba yake mpya, ambayo sasa inaelea kwenye mto unaoitwa River Ouse huko North Yorkshire.

Hii imemfanya kupata nyumba bure isiyomlazimu kulipia pango ama kodi. Hapo awali aliishi katika nyumba ndogo huko Bedford, ambayo aliifanyia ukarabati - na kuongeza thamani yake - na kisha kuiuzwa.

Mara baada ya kontena la meli lililoharibiwa, ambalo lilikuwa limesafiri sehemu nyingi duniani, alilirekebisha na kulibadilisha kuwa nyumba yake ya boti, McMurdo pia alitimiza ndoto ya muda mrefu ya kuishi karibu au juu ya maji: "Siku zote nilikuwa na ndoto ya kuishi karibu na maji katika nyumba ndogo,” anasema.



Mnamo mwaka wa 2018, Agnès Combes Bernageau alihama kutoka nyumba yake "nzuri ya ghorofa" huko Paris hadi kwenda kuishi kwenye jahazi, ambapo anaishi na watoto wake wawili na mbwa 'bulldog' mwenye asili ya Ufaransa.

Nyumba yake hiyo (Jahazi) mpya ina historia ya kupendeza: ilijengwa mnamo 1930 huko Mainz, Ujerumani, kisha ikakabidhiwa kwa Ufaransa kama sehemu ya malipo ya baada ya Vita vya Kwanza vya dunia kwa mujibu wa Mkataba wa wa Versailles wa mwaka 1919.

"Nilichoshwa na maisha yasiyo ya faragha ya Paris," anasema Combes Bernageau, ambaye ameibadilisha boti hiyo na kuiremba kuwa nyumba ya kuvutia.



Kuishi kwenye nyumba ya boti wakati mwingine kunaweza kuchochewa na uamuzi uliopo wa kuachana na maisha marefu kwa mtu anayeleta uamuzi mkubwa zaidi unaoishi maisha binifasi. Anibal Guiser Gleyzer ni mfano halisi. Miaka 30 hivi iliyopita, alikutana na maisha ya kuishi mjini yasiyoridhisha. "Kwa hivyo nilinunua mashua na kufanya ufafiti kwenye fukwe ya mito ya Paraná na Uruguay," anasema. Baadaye aliuza nyumba yake yake ya gorofa, iliyokuwa karibu na fukwe, akijua kwamba ardhi oevu katika eneo ilipokuwa ghorofa lake inakabiliwa na mafuriko, akaamua kujenga nyumba inayoelea.

Zazi Houseboat, Uholanzi

Kwa miaka mingi Jeanne de Kroon, ambaye ana biashara ya mavazi ya zamani inayoitwa Zazi Vintage, alisafiri ulimwenguni kote, akitafuta nguo zilizobuniwa na kutengenezwa kawaida na mafundi. Lakini hivi majuzi alikata mzizi wa fitna kukodisha nyumba ya mashua katika kitongoji cha Amsterdam. "Kwa wasafiri, boti ya nyumbani ndiyo njia kuu ya kujisikia kama uko likizoni lakini nyumbani," anasema de Kroon, anayevalia mavazi ya hippy ya mtindo wa miaka ya 1960.

Maisha ya kuishi kwenye mashua inatufanya wenfine tuwe jumuiya ya pamoja - tunapeana zawadi na tumekuwa na klabu ya kuogelea - Jeanne de Kroon

Anaishi kwenye boti ya mbao iliyotengenezwa miaka ya 1970. De Kroon alichokifanya ni kuiongeza rangi, kuiremba kwa nguo za zinazoning'inia. Ina muonekano wa kiasili. "Unapoishi kwenye mashua kwenye mito na mifereji mikubwa ya Amsterdam, rangi ni muhimu ili kuongeza joto," anasababu.

Oldenburg, Denmark



Wakati Lis na mwenza wake Ove Nilsson walipoona mashua iliyogeuka nyumba yao huko Oldenburg, ambayo iliundwa mwaka 1908, walivutiwa na ukubwa wake - waliona inafaa kuishi na kukaribisha familia zao na marafiki.

Ni nyumba inayoelea na kutembea, imeundwa eneo kubwa la kulia chakula, ina jiko, vyumba viwili vya kulala, bafui na sehemu kubwa inayokuruhusu kutembea.

Sakafu yake ni iliyopauka lakini mpangilio wa vitu vya ndani (samani au fenicha) zenye umbo la meli, ni za hali ya chini lakini za kustarehesha. Kuna sofa kubwa na viti virefu kwenye eneo la kulia, huku vyumba vikinakshiwa kwa mbao za kitamaduni zilizong'arishwa.

"Hatujakosa chochote kwa kuhama kutoka nchi kavu hadi kuja kuishi majini," wanasema. Tangu kuhamia kwenye nyumba hiyo Oldenburg, wanandoa hao wameenda kwenye safari nyingi za meli, haswa kwenye pwani ya magharibi ya Jutland.

Soggybottom Shanty, Marekani



Uzoefu mzuri wa Siva Aiken, mmiliki wa boti iliyogeuzwa nyumba inayoitwa kwa kifupi Soggybottom Shanty, ilikuwa ni safari yake akiwa huko Anaheim, ambayo familia yake ilitembelea wakati wa utoto wake.

Boti yake ya urefu wa mita 7 ilitengenezwa kwa vifaa vilivyosindikwa na kutupwa, kwa usaidizi kutoka kwa marafiki, mwaka wa 2019. Madirisha yake ni yale yaliyotupwa baada ya kutolewa kwenye nyumba iliyokuwa imeeekwa madirisha mapya, huku injini yake ikiwa ni ya 'mtumba' yenye umri wa miaka 30.

Altar, Brazil



Kwa Rodrigo Martins, familia yake na marafiki wawili, boti yao ya mazingira tulivu lakini kubwa, iliyo nje ya gridi ya taifa - iliyowekwa kwenye boya kwenye bwawa la Jaguariuna saa mbili kutoka kaskazini mwa jiji la São Paolo - ni ndoto nzuri.

Boti hii yenye muundo mdogo wa 38m-sq ilitengenezwa kwa kutumia vifaa vyote vilivyorejeshwa upya kwenye matumizi. Ni mfumo wa makazi uitwao LilliHaus, uliotengenezwa na Brazil sysHaus. Kuna viti juu yake, ambapo baada ya jua kuzama, watu wanaweza kutoa na kukaa hapo kutazama sinema zinazoonyeshwa kwenye ukuta wa nje uliotengenezwa kama 'skrini' ya sinema.

De Walvisch, Uingereza



Nyumba ya De Walvisch, meli ya meli ya Uholanzi, ambayo sasa imetia nanga Wapping, London Mashariki, ni ya kuvutia. Inajivunia kuta za mbao zenye uzito mkubwa na wingi wa vitu vya kuvutia vilivyo na asili ya zamani ya baharini. Watu wanaoishi numo ni - wasanii Zatorski & Zatorski (wanandoa ambao marafiki zao wanawaita Thomas na Malaika).

Mnamo 2000, wawili hao walinunua mashua hiyo nyembemba, baadae kuiboresha". Uamuzi wao wa kununua De Walvisch uliimarishwa na nia yao ya kuhamia majini na kuishi wakielea. "Historia iko kila kona katika sehemu hii ya mji," wanasema.

Wenza hao walirejesha mashua hiyo, na kuitengeneza kwa vipande vilivyorejeshwa, kuongeza nakshi. Mlango wake wa shaba - ulitoka SS Transylvania, meli ya abiria wa Uingereza ambayo ilizamishwa na mashua ya Ujerumani mnamo 1917 - sasa unapamba chumba cha kulala (zamani kilitumiwa na nahodha wa meli).

MWISHO.

Source: BBCSwahili

Post a Comment

Previous Post Next Post