UVCCM ZANZIBAR YATEMBELEA VIKUNDI VYA WAJASIRIAMALI







Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM Taifa ikiongozwa na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Komredi Mohammed Ali Kawaida imetembelea vikundi vya wajasiriamali na kukutana na timu za mpira zitokanazo na vikundi mbalimbali.

Kamati ya utekelezaji ikiongozwa na Mwenyekiti wametoa jezi peya tatu (3) za jezi na mipira sita (6) ili vijana waendelee kuimarisha vipaji vyao, pia wametoa kiasi cha fedha kwa vikundi vya ujasiriamali ili kuwaongezea mtaji na kutanua wigo wa biashara zao.

Lengo kuu la ziara ya kamati ya utekelezaji ni kuimarisha Uhai wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana, kutembelea miradi inayohusisha utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2020 - 2025 pamoja na miradi ya Chama na Jumuiya zake.

Post a Comment

Previous Post Next Post